
Na John Mapepele, Birmingham Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona ili kurejea na medali. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa kwa ujumla. "Nawaomba tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita tunahitaji kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha, amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua na kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa. " kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali imeamua kutoa fedha nyingi kwa w...