Siku ya kiswahili yafana

 



Na John Mapepele

Mamia ya wadau leo Julai 7, 2022 wameshiriki maadhimisho ya kwanza ya siku ya Kiswahili duniani jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho haya  yanafanyika  kwa mara ya kwanza kufuatia  UNESCO kuridhia kiswahili kuwa lugha rasmi kuwa lugha kutumika kimataifa.

Mgeni rasmi wa shughuli hii, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Isdor Mpango.

Mhe. Mpango mara baada ya kufika ametembelea maonesho ya wadau mbalimbali wa kiswahili ambao wamekuwa wakionesha kazi za kiswahili.



Wadau mbalimbali wa kiswahili wametoa mada na shuhuda za ukuaji wa kiswahili kwa lugha ya kiswahili.

Washiriki wamepongeza kwa watoa mada na mashuhuda wote kutoka ndani na nje ya Tanzania waliopanda kuzungumza kwa kusema vizuri lugha ya kiswahili.

Kaulimbiu  ya siku hii ni " kiswahili ni chachu ya maendeleo na utengamano duniani "

Comments

Popular posts from this blog

BODABODA SINGIDA WATOA TAMKO KALI KUELEKEA KUAPISHWA RAIS DKT JOHN MAGUFULI

RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI

AGIZO LA MAGUFULI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA BI ELIZABETH MANYONI LATEKELEZWA 100%