Mhe. Mchengerwa amkabidhi bendera Mpoto

 

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa  na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amemkabidhi bendera ya Taifa msanii nguli nchini Mrisho Mpoto  aliyechanguliwa na UNESCO kushiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani huko Paris  Ufaransa.

Akikabidhi bendera hiyo kwa Mpoto akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara yake. Dkt,  Hassan Abbasi amemtaka Mpoto  kuliwakilisha vema  Taifa wakati atakapopanda na kughani mashairi ya Kiswahili katika siku hiyo.

Amesema kiswahili ni miongoni mwa lugha pekee afrika ambayo inazungumzwa na waafrika na imekubalika kuzungumzwa katika mikutano ya kimataifa.

Aidha, amesema fursa na heshima aliyoipata kutoka UNESCO ni kubwa hivyo kazi yake sasa ni  kuhakikisha kuwa anaitangaza Tanzania kupitia lugha ya kiswahili ili nchi mbalimbali za duniani zikiwa na hitaji la wataalam wa kiswahili waje Tanzania  kuwapata wataalam hao.

Amesema ili kuhakikisha lugha ya kiswahili inapata heshima inayostahili Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya maadhimisho ya wiki nzima ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa Julai 7 na Makamo wa Rais. Mhe, Dkt. Isdor Mpango anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi.


Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuenzi lugha ya kiswahili kwa kuwa Tanzania ndiyo chimbuko la kiswahili.

Naye Mpoto ameishukuru Serikali kwa jitihada kubwa inayofanya kwa kuwasaidia wasanii na kuendeleza lugha ya kiswahili.

Amesema anatambua heshima kubwa aliyopata kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya kiswahili na kwamba ataiwakilisha vema Tanzania.

Kwa upande wake, Dkt. Abbasi amempongeza Mpoto na kuwataka wasanii wengine nchini kubadika na kutumia kiswahili sahihi katika kazi zao.


Comments

Popular posts from this blog

BODABODA SINGIDA WATOA TAMKO KALI KUELEKEA KUAPISHWA RAIS DKT JOHN MAGUFULI

RAIS SAMIA AZIDI KUKIPAISHA KISWAHILI DUNIANI

AGIZO LA MAGUFULI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA BI ELIZABETH MANYONI LATEKELEZWA 100%