Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia upya kanuni kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sanaa nchini Tanzania ili ziweze kuainisha bayana mfumo mzuri wa ufanyaji kazi unaowashirikisha wasanii binafsi, vyama, na mashirikisho ya Sanaa. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Mirabaha kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka iliyoongozwa na Victor Tesha. “Mfumo huu utasaidia kuwatambua wasanii wote nchini na kuweza kuwahudumia kwa urahisi kwani mfumo uliopo sasa unatoa nafasi ya kila msanii kujitafutia riziki mwenyewe kitu kinachofanya wasanii wengi kukosa umoja na kuzalisha migogoro isiyokuwa na tija”. Amesisistiza Mhe, Mchengerwa Pia...
Popular posts from this blog
Mhe.Mchengerwa ampokea Rais wa FIFA
Na John Mapepele, Arusha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa usiku huu ameongoza ujumbe wa kumpokea Rais wa FIFA Gianni Infantino anayekuja kuhudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF). Mkutano huo wa kwanza wa kihistoria unafanyika kwa mara ya kwanza nchini huku zaidi ya nchi 58 kutoka sehemu mbalimbali duniani zikishiriki. Mhe. Mchengerwa amemkaribisha Rais wa FIFA Gianni na kumpatia salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumwelezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ambapo Rais wa FIFA ameelezwa kuridhishwa na maendeleo ya Michezo. Amepongeza kazi kubwa huku akisema amefurahishwa na makaribisho hayo. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na kuangaliwa na watu zaidi ya bilioni moja. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa anatarajiwa kumwakilisha Mhe. Rais. Katika mkutano huo CAF inakwenda kuzindua mashindano maalum ya soka y...
RUBI, NANDY JUKWAA MOJA LEO TANZANITE FESTIVAL DAR
Msanii Ruby Msanii Nandy Na John Mapepele,Dar Wasanii mahiri wa kike ambao pia wamekuwa katika ushindani kimuziki Rubi na Nandy leo wataonesha kuwa wanawake wakiwa na lao wanaungana. Baada ya miaka mingi ya kukwepana na kila mmoja kuonekana anapania kufanya vizuri zaidi ya mwenzake leo Jumamosi, Septemba 18, 2021, Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite linawakutanisha kwenye Uwanja wa Uhuru hapa Dar es Salaam. Michezo mingi leo ikiwa ni siku ya tatu tayari imeanza asubuhi na itaendelea hadi jioni ambapo saa kumi jioni Simba Queen itaoneshana ubabe na Timu ya Taifa ya Wanawake U23 kwenye Uwanja huo wa Uhuru. “Wasanii zaidi ya 10 watakaopanda stejini leo wakiwemo Nandy na Rubi watu wajazane uwanjani kabla ya saa nane kwani baada ya hapo kutakuwa na ufunguzi na wasanii hawa watatumbuiza mpaka jioni,” ametangaza MC wa sherehe hizo jana jioni wakati wa mapambano ya ndodi uwanjani hapo. Wasanii wengine wakali wa kike wanaotarajiwa kuwepo leo (wakisindikizwa na kaka yao mkali...
Comments
Post a Comment