SANJAY DUTT KUWASAIDIA WASANII KUITANGAZA TANZANIA -MHE BASHUNGWA

Picha
ya pamoja baina ya Mhe. Innocent Bashungwa na Sanjay Dutt Viongozi
mbalimbali kwenye Sekta Sanaa na wasanii (waliosimama nyuma)

Innocent Bashungwa(kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili Sanjay Dutt


Wasanii mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Sanjay Dutt
*********************************
Na John Mapepele, WUSM
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Innocent Bashungwa amesema
mwigizaji maarufu duniani kutoka nchini India Sanjay Dutt amekubali
kuwasaidia Wasanii wa Tanzania katika maeneo ya kuandaa filamu, vifaa na
utaalam ili kutangaza utalii wa Tanzania duniani.
Akizungumza
kwenye Mkutano wa kumtambulisha Dutt kwa Waandishi wa Habari na wadau
mbalimbali wa Sanaa na Filamu nchini leo Novemba 11, 2021 jijini Dar es
Salaam. Mhe, Bashungwa amefafanua kuwa Msanii Dutt amekubali kuleta
wataalam ambao watashirikikiana na Bodi ya Filamu, Taasisi ya Chuo cha
Sanaa Bagamoyo na Kampuni ya Africable katika kuwasaidia wasanii wa
Tanzania katika maeneo mbalimbali.
“Ujio
wake ni fursa kwa nchi yetu na kunatusaidia kuendeleza safari ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya
kuitangaza Tanzania kupitia filamu, safari ambayo Mhe. Rais aliianza
kupitia maandalizi ya filamu ya Royal Tour” Ameongeza Mhe. Bashungwa
Amesema
ujio huu unaashiria kuwa tasnia ya filamu nchini Tanzania, inapitia
mabadiliko chanya na makubwa, kiasi kwamba waigizaji wakubwa wa filamu
kama Dutt, wanasikia furaha na kutenga muda kutembelea Tanzania na kuwa
uwepo wake hapa utakuwa ni fursa kubwa kwa tasnia ya filamu na wadau
wote wa filamu nchini.
Aidha,
Mhe. Bashungwa ametumia muda huo kumwomba Msanii Sanjay Dutt kutoa
vifaa vya kuandaa filamu za kisasa kwa wasanii wasio na uwezo wa kuwa na
vifaa hivyo na kwamba vitakuwa vikitunzwa na kusimamiwa na Bodi ya
Filamu nchini na Msanii huyo amekubaliana na ombi hilo.
Pia,
Mhe. Bashungwa amefafanua kuwa Sanjay Dutt amesema anakusudia kuandaa
filamu kubwa ambayo itaisambaza duniani kwa ajili ya kuitangaza
Tanzania.
Akizungumza
kwenye mkutano huo Msanii Sanjay Dutt amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu kwa
ukaribisho ambapo ameahidi kuisaidia Tanzania kuwa katika sura ya dunia
kwenye tasnia ya filamu.
Pia
ametoa wito kwa Serikali kuwa “film academy” ambayo itasaidia kuandaa
fani mbalimbali kama uigizaji na muziki ambapo amekubali kuwaleta
wataalam kutoka India kuja kufundisha.
Comments
Post a Comment