TAMASHA LA KIHISTORIA LATUA MBEYA-BASHUNGWA
Na. John Mapepele, WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Filamu nchini inatarajia kwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru wake kufanya tamasha kubwa la kihistoria la utoaji wa tuzo mbalimbali za filamu ambalo litafanyika Disemba 18, 2021 jijini Mbeya. Akizungumza na kwenye Mkutano wa Waandishi wa wa habari jijini Mbeya, Novemba 29, 2021 Mhe. Bashungwa amesema sababu kubwa ya kufanyia kilele cha tuzo hizi jijini Mbeya ni kutambua uwepo wa wanatasnia ya filamu pamoja na wasanii katika mikoa na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam ili kuamsha ari ya kufanya kazi za sanaa na hatimaye kujipatia ajira na kipato kitakacho boresha maisha yao. “Tamasha hili linakwenda kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko maeneo hayo katika uwanja huu wa filamu na Sanaa kwa ujumla kupitia idadi kubwa ya wapenzi wa filamu watakaokuwa wanafuatilia tukio hili ...