RAIS SAMIA AMWAGA MABILIONI UJENZI WA OFISI ZA SANAA NA MICHEZO
Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akionesha picha ya jenhgo jipya la Wizara hiyo mara baada ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Septemba 22,2021 jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi(kulia) wakikabidhiana Mikataba ya Ujenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani. Picha ya pamoja baina ya Katibu Mkuu na Menejimenti ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo katika pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) …………………………………………………………………………… Na John Mapepele- WSUM, Dodoma Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kujengewa jengo la TZS Bilioni 22.843 makao makuu jijini Dodoma na mkataba wa ujenzi tayari umesainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani. Akizungumza katika hafla hiyo y...