
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia upya kanuni kwa kuwashirikisha wadau wote wa Sanaa nchini Tanzania ili ziweze kuainisha bayana mfumo mzuri wa ufanyaji kazi unaowashirikisha wasanii binafsi, vyama, na mashirikisho ya Sanaa. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa rasmi ya namna bora ya ya kusimamia HAKIMILIKI na Mirabaha kwa wasanii nchini kutoka kwa Kamati aliyoiteua Julai Mosi mwaka iliyoongozwa na Victor Tesha. “Mfumo huu utasaidia kuwatambua wasanii wote nchini na kuweza kuwahudumia kwa urahisi kwani mfumo uliopo sasa unatoa nafasi ya kila msanii kujitafutia riziki mwenyewe kitu kinachofanya wasanii wengi kukosa umoja na kuzalisha migogoro isiyokuwa na tija”. Amesisistiza Mhe, Mchengerwa Pia...