Posts

Showing posts from May, 2022

Mhe. Mchengerwa awakabidhi kombe la UEFA mashabiki wa Real Madrid

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewakabidhi kombe la UEFA mashabiki wa timu ya Real Madrid baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa usiku wa kuamkia leo huku akisisitiza kuwa  Wizara yake itaendelea kuwa bunifu kwenye sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwapa furaha watanzania. Mhe. Mchengerwa amesema hayo kwa wapenzi soka  katikati ya Daraja  la Tanzanite jijini Dar es Salaam kwenye tukio maalum la kuangalia mubashara fainali za UEFA lililoratibiwa na kampuni ya kinywaji cha  Heineken kwa  kushirikiana na Wizara  ya Utamaduni, Sanaa na Michezo usiku wa kuamkia leo. Katika fainali hii timu ya Real Madrid imeibuka bingwa wa  kombe la UEFA wa mwaka huu baada ya kuibamiza Liverpool bao moja katika kipindi cha pili cha mchezo. Ameongeza kuwa  sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo nguvu shawishi za taifa lolote duniani. Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Has...

Waziri Mchengerwa atema cheche kwa viongozi wa michezo, ataka wabadilike

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa amewataka  viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini kutotumia taasisi wanazoziongoza kujinufaisha kwa  vipato tu na badala yake wawe wabunifu na wazalendo ili kuleta  mapinduzi kwenye  michezo  na kuendana  na maono ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ya kutumia michezo kuleta uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Mei 27, 2022 wakati akifunga  kikao kazi cha viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini  kilichoratibiwa  na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufuatia  maelekezo yake aliyoyatoa wakati akiisimika Bodi  ya BMT hivi karibuni ya kutaka kuwa na utawala bora kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili kuendeleza michezo. Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa yapo  mataifa  mbalimbali duniani ambayo  hayana miundombinu ya michezo na...

MHE. MCHENGERWA- TANZANIA YAANZA MAANDALIZI YA KURATIBU AFCON

Image
  Na John Mapepele Serikali ya Tanzania na Qatar imefanya mazungumzo ya kuimarisha mahusiano kwenye sekta za michezo, sanaa na utamaduni ambayo  yanalenga kusaidia Tanzania  kufanya mapinduzi makubwa  kwenye sekta za michezo nchini ikiwa ni pamoja na Tanzania kuratibu mashindano makubwa ya Afrika ya Soka hususan Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ifikapo mwaka 2027. Maongezi hayo yamefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa kwa upande wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Hussain Ahmad Al-Homaid leo Mei 27, 2022 Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Mhe. Mchengerwa amefafanua kuwa tayari Serikali imeshaomba  miundombinu ya soka inakayotumika kwenye  mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajiwa  kufanyika nchini Qatar ambapo Mhe, Balozi Al-Homaid amesema  Serikali yake itazingatia  ombi hilo kwa kuipa kipaombele nchi ya Tanzania. “Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Sam...

Mhe. Mchengerwa atoa neno siku ya Utamaduni wa vyakula vya asili vya Uturuki

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Mei 26, 2022  amehudhuria  kilele cha siku ya Utamaduni wa vyakula vya asili vya Uturuki kwenye ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam pamoja na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Uturuki kwenye sekta za Utamaduni na Sanaa kwa faida ya nchi zote mbili. Mhe. Mchengerwa amesema ameishukuru Serikali ya Uturuki kwa kujenga kituo cha utamaduni hapa nchini. Amesema Tanzania itaendeleza  ushirikiano huo kwenye sekta ya Utamaduni ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika eneo la wataalam wa Utamaduni. Aidha amepongeza Uturuki kuendelea kutangaza lugha ya kiswahili duniani kupitia filamu zao zinazotafriwa kwa lugha ya kiswahili. Ameongeza kuwa mwaka huu, Tanzania inakwenda kuadhimisha siku ya kiswahili duniani kuanzia Julai mosi hadi kilele chake Julai saba  kwa kufanya program mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya maon...

MHE. MCHENGERWA AONGOZA TANZANIA KUSAINI MIKATABA YA SEKTA ZA UTAMADUNI NA SANAA NA CHINA

Image
  Na John Mapepele. Serikali ya Tanzania na China leo, Mei 26, 2022 zimetiliana Saini mkataba wa makubaliano ya kusaidiana katika kuboresha maeneo ya Sekta anazozisimamia. Utiaji wa Saini wa mikataba hiyo ya kihitoria umeongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mhamed Omary Mchengerwa kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Balozi wa China nchini Wang Ke  kwa upande wa Serikali ya watu wa China kwenye Ofisi ya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam. Akizungumzia kuhusiana na manufaa ya mikataba hiyo, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania imesaini mikataba hiyo ya ushirikiano inatarajia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo. Amesema kwa upande wa utamaduni  kutakuwa  na kupeleka wadau wa utamaduni, sanaa na michezo katika nchi ya  china na watu wa china kuja  nchini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu. Kwa upande wa elimu Tanzania itapeleka wanafunzi ambapo China itafadhili  masomo haya kwa kutoa nafasi ...

Mhe. Mchengerwa Atoa salamu Siku ya Afrika

Image
  Na Shamimu Nyaki - WUSM, Dodoma  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.  Mhe, Mohammed Mchengerwa amewaasa watanzania kulinda na kuhifadhi rasilimali na kumbukumbu ambazo ni ushahidi wa Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika katika maeneo waliyopo ambayo kumbukumbu hizo zinapatikana. Katika taarifa aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari leo  Mei 25, 2022 jijini Dodoma, Mhe. Mchengerwa amesema  Siku ya Afrika ambayo huazimishwa Mei 25 kila Mwaka,ni siku muhimu kwa waafrika wote ambapo kwa mwaka huu  imebebwa na Kauli Mbiu isemayo "Urithi wa Ukombozi, Fahari ya Afrika na Kazi Iendelee". "Kuthamini utanzania wetu  ni jambo la msingi na ndiyo kielelezo na sifa iliyosababisha Umoja wa Afrika (AU) zamani (OAU) kuichagua Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika na kuipa hadhi ya kuwa Mratibu wa Harakati za Ukombozi hadi nchi zote za Afrika zilipopata Uhuru mwaka 1994" amefafanua Mhe.Mchengerwa. Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, ni wajibu wa ...

Halima Kopwe Miss Tanzania 2022, Rais Samia kujenga ukumbi wa kimataifa jijini Dar

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Mhe. Rais Samia imedhamiria kuinua kuinua kiwango cha mashindano ya urembo nchini  ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi wa kimataifa  katika jiji la Dar es Salaam. Akizungumza usiku wa kuamkia leo Mei 21, 2022 kwenye kilele cha mashindano ya kumtafuta  Miss Tanzania 2022 ambapo Halima Kopwe toka Mtwara ametwaa taji hilo, Mhe . Mchengerwa amesema ukumbi huo  licha ya kufanyiwa kazi mbalimbali za Sanaa na burudani pia utatumika kwenye mashindano ya kimataifa ikiwa ni pamoja na shindano la Miss Tanzania. "Ukumbi huo unatarajiwa kuongoza kwa ubora na ukubwa barani Afrika ambapo utachukua takribani watu elfu ishirini" amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha, amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuwashika mkono washindi wote na kufafanua kuwa washiriki wote walioshiriki shindano hili hadi kufika fainali ni washindi. Amewapongeza waandaji wa shindano hilo kwa uratibu mz...

UEFA LIVE DAR-MHE. MCHENGERWA

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kilele cha mashindano ya 67 ya UEFA baina ya Timu ya Real Madrid na Liverpool yataoneshwa mubashara nchini kwenye daraja jipya la Tanzanite jijini Dar es Salaam kupitia DStv  ambapo vivutio mbalimbali vya utalii vitaonyeshwa  moja kwa moja  hivyo kutoa fursa kwa mamilioni ya wapenzi wa soka kutoka nchi zote za Afrika na dunia kushuhudia shindano hilo na vivutio vya utalii kutoka Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Powerbreakfast kinachorushwa na kituo cha Redio cha Clouds Fm leo Mei 17, 2022 jijini Dar es Salaam. Mhe, Mchengerwa amesema mbali na  kurusha mubashara  mechi hiyo yenye mvuto mkubwa  hapa nchini na duniani kote pia Filamu ya Royal Tour itaonyeshwa  kabla  ya kuanza  kwa mechi hiyo ambapo ametoa wito kwa  wananchi kujitokeza  kushuhudia  tukio hilo la kihistoria. Amefafanua kuwa wakati wa Filamu hiyo ya kihistoria iliy...

Mhe. Mchengerwa awataka watoa huduma kwenye sherehe kuwa wabunifu

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema huu ni wakati wa kuongeza ubunifu kwenye utendaji kwa tasnia ya utoaji wa huduma katika sherehe  ili kutoa ajira na kuongeza vipato vyao kwa ujumla.   Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo leo Mei 15, 2022  kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye kilele cha maonesho  ya tano ya biashara yanayowajumuisha  watoa huduma wote kwenye sherehe baada ya kukagua mabanda yote ya washiriki. Watoa huduma hao ni pamoja na washereheshaji, wauzaji wa nguo za harusi, wapishi, wapiga picha wenye saloon na watengenezaji keki. Aidha, amewaomba watumie mashirikisho yao ili iwe rahisi kwa Serikali kutatua changamoto zinaziwakabili. Kuhusu Serikali kutoa  mikopo kwa watoa huduma amesema tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa  1.5 bilioni kwa ajili yao  na kuwaomba   kuwasilisha maandiko  Serikalini kupitia  mas...

Serikali yawaomba Machifu na Viongozi wa Kimila kushawishi jamii zao kushiriki Sensa

Image
  Na. John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  ametoa wito kwa Machifu wote nchini na Viongozi wa  Kimila kuhakikisha wanawashawishi watu wote kwenye jamii zao ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu kuhesabiwa kwenye zoezi la kitaifa la sensa ya sita ya watu itakayofanyika  Agosti 23, 2022 nchi nzima ili kuisaidia Serikali kuweza kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake. Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Mei 7, 2022 kwenye  ufunguzi wa mkutano wa Machifu na Viongozi wa Kimila  kutoka mikoa yote hapa nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salam.   Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa viongozi hao na kwamba  itaendelea kuwaheshimu, kuwajali na kuwasikiliza viongozi ili kuweza kujifunza  mambo kupitia kwao ambapo amesisitiza kwamba mtu yoyote atakayejaribu kuwadharau viongozi  hao atachukuliwa hatua.  “Sisi wa...

TaSUBa washindi Uni Tarent 2022, wazoa milioni kumi, Serikali kuwapiga msasa bure washiriki wote

Image
  Na. John Mapepele  Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali kupitia Wizara imewatunikia zawadi ya kupewa mafunzo maalum ya fani za washiriki wote wa Uni Talent Show wa 2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili wapigwe msasa kuongeza ubunifu katika sanaa zao. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Mei 7, 2022 kwenye kilele cha shindano hilo la wasanii  kutoka vyuo mbalimbali nchini la Uni Talent Show  katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Amepongeza waandaaji wa shindano  hilo na kufafanua kuwa Serikali  ya Awamu ya Sita  ina dhamira ya dhati ya kuinua na kukuza  taaluma na kazi za wasanii ili waweze kufaidika  na kazi zao.   Kikundi cha African Cousins kinachoundwa na vijana sita kutoka TaSUBa kimeibuka Kinara katika mashindano ya vipaji kwa wanavyuo ya Uni Tarent. Kikundi hicho kimeibuka kinara dhidi ya washindani wake 12 kutoka vyuo mbalimbali...