Posts

Showing posts from December, 2021

Waziri Bashungwa Afanya Tathimini Mechi Ya Burundi, Aipa Tanzanite Silaha Za Maangamizi Mechi Ya Ethiopia .

Image
  Na John Mapepele, WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake U20 ya Tanzanite kwa kuendelea kufuzu tiketi ya kucheza mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2022 nchini Costa Rica baada ya kushinda goli 1-1 na timu ya Burundi licha ya kucheza wachezaji pungufu( wachezaji nane tu) disemba 18, 2021 nchini Burundi. Kufuatia ushindi huo leo disemba 21, 2021ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuijenga kimwili na kisaikolojia kuelekea mchezo unaifuata dhidi ya timu ya Ethiopia mapema Januari 2022. “kwa niaba ya Serikali ninawapongeza sana kwa kuwa mliishangaza Afrika na Dunia, mlicheza pungufu lakini bado tukapata ushindi wa heshima, jambo muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo mechi inayofuata januari na kazi iendelee" amefafanua Mhe. Bashungwa, leo Desemba 21, 2021 alipokutana na timu pamoja na kamati ya ufundi na kufanya tathimini mchezo...

WAZIRI BASHUNGWA AITAKA MIKOA KUSHIRIKIANA NA WIZARA KUANDAA TUZO ZA FILAMU

Image
  OHN MAPEPELE–WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa mikoa yote nchini kuiga Mkoa wa Mbeya katika kushirikiana na  Wizara yake  kuandaa Tuzo za Filamu katika miaka ijayo ili kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasanii wengi zaidi walio kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini. Mhe. Bashungwa ametoa kauli hiyo Jijini Mbeya katika kilele cha utoaji wa Tuzo za Filamu nchini iliyoratibiwa na Bodi ya Filamu chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Disemba 18, 2021. Mchakato wa kutafuta filamu hizo bora umechukua zaidi ya miezi mitatu. “Ndugu yangu Comrade Juma Zuberi Homera, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nakupongeza sana kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu chini ya usimamizi wa wizara yangu.”amesisitiza Mhe. Bashungwa Mhe. Bashungwa amesema kufanyika kwa tamasha hili la kwanza katika historia ya Tanzania kabla na baada ya  uhuru ni utekelezaji wa  azma ya Serikali ya kushirikisha wadau, kurejesha utamaduni wa kutoa tuz...

Vyama Vya Michezo Tumieni Taifa CUP Kuwapata Wachezaji Bora Wa Taifa- Bashungwa

Image
  Na John Mapepele. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent l. Bashungwa ametoa wito kwa vyama vya kitaifa vya michezo, kutumia mashindano ya Taifa CUP 2021 kuchagua vipaji vya wachezaji na kuviendeleza ili kupata vipaji vitakavyounda timu za Taifa za michezo mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Mhe. Bashungwa ameyasema hayo, leo Desemba 10,2021 wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.  Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania, wanashiriki kikamilifu katika shughuli za michezo kwa kuwa michezo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi hususan kwenye Marnie ya uchumi, siasa na jamii. “Kimsingi michezo ni ajira, amani, mshikamano, afya na furaha. Kutokana na umuhimu huu wa sekta ya michezo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeamua kwa dhati kabisa, kwa kusaidiana na Vyama vya Michezo chini ya Baraza la Michezo la Taifa, kuanzisha shindano la Taifa Cup ambalo lil...

MHE.BASHUNGWA KUFUNGUA TAIFA CUP LEO, WASANII LUKUKI KUCHAGIZA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan Waziri wa UTamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi Bahati Bendi ni miongoni mwa wasanii wataokuwepo. ……………………………… Na. John Mapepele Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa (Mb) leo Desemba 10, 2021 anazindua Mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mhe. Bashungwa amesema Serikali imeamua kufufua mashindano hayo ili kupata vipaji vya wachezaji ambavyo vitaendelezwa ili Tanzania iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya kimataifa.  “Lengo la mashindano hayo pia ni kuwashirikisha wanamichezo kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.Tunatarajia yatasaidia  kuleta umoja na mshikamano, kutoa ajira na kuimarisha afya za wachezaji wetu. Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejesha mashindano hayo ambayo yaliku...

Rais Samia- Miaka 60 ya uhuru, Kiswahili kimekua kimataifa.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Innocent Bashungwa. Na. John Mapepele  Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru leo Disemba 9, 2021 amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye lugha ya Kiswahili. Rais Samia ameyasema haya jana usiku Disemba 8, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wananchi ambapo alieleza pamoja na mambo mengine mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania. “Nchi nyingi zinatumia lugha za kigeni kama lugha za mataifa yao zinazowaunganisha, inapendeza kuona kuwa tunatimiza miaka 60 tukiwa wamoja wenye utambulisho mmoja na lugha moja ya Kiswahili inayoendelea kupata umaarufu kimataifa   siku hadi siku”. Amefafanua Rais Samia. Amesema wakati Tanzania ilipopata uhuru Kiswahili haikuwa lugha inayozungumzwa na watu wote ndani ya Tanganyika bali kizazi kilichofuata baada ya uhuru wal...

GEKUL-DROO YA UPANGAJI WA MAKUNDI YA TIMU NA RATIBA TAIFA CUP YATOKA

Image
  Shafi Dauda (kushoto) na Baraka Kizuguzo ambaye ni Afisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) wakichezesha droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano ya Taifa CUP 2021 Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul akishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam. Kushoto Kaimu Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa. Bi Neema Msita, kulia Mkurugenzi wa Michezo. Yusu Omary Singo. Wadau wa michezo wakishuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam. ******************** Na. John Mapepele Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul leo, Disemba 8, 2021 ameshuhudia droo ya upangaji wa makundi ya timu na ratiba ya mashindano Taifa CUP 2021ambayo yanatarajia kuanza Disemba 10, 2021 jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika tukio...

RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA KUIPELEKA TIMU YA WENYE ULEMAVU KOMBE LA DUNIA

Image
   Na. John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itahakikisha  inaendelea kuitunza na kuijengea mazingira mazuri timu ya Taifa ya Soka ya wenye ulemavu (Tembo Warriors) iliyofuzu kucheza kombe la dunia mwakani Oktoba 2022 nchini Uturuki ili iweze  kufanya vizuri katika mashindano hayo. Mhe. Rais ameyasema haya leo Disemba 7, 2021 Ikulu ya Dar es Salaam kwenye hafla maalum aliyoialika timu ya Tembo, kufuatia kufanya vizuri katika mashindano ya soka ya Afrika ya wenye ulemavu (CANAF 2021) yaliyoisha hivi karibuni jijini Dar es Salaam  na Tembo Warriors kufuzu kuingia kwenye kombe la  dunia  baada ya kushika nafasi ya nne.  “Niwapongeze watoto wangu mmekonga nyoyo na mmetoa somo kwamba mnaweza pia mmeandika historia” amesisitiza Mhe. Rais Samia.   Rais Samia ameishukuru na kuipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha maandalizi ya mash...

SINGO- MAANDALIZI MECHI MIAKA 60 YA UHURU, TANZANIA NA UGANDA YAMEKAMILIKA

Image
    ********** Na. John Mapepele Serikali imesema kuelekea kilele cha maadhimishio ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania maandalizi ya mchezo wa soka wa kirafiki baina ya timu ya Tanzania na Uganda kwa wasichana na wanaume itakayochezwa siku ya kilele cha maadhimisho hayo Disemba 9, 2021 yamekamilika. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo nchini, Yusufu Omary Singo leo, Disemba 7, 2021 kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Singo amesema timu zinatarajiwa kuwasili nchini lwo Disemba 7, 2021 tayari kwa mechi zote zitakazochezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo mchezo utakaoanza ni kwa timu ya wanawake utakaochezwa majira ya saa 11:00 jioni na mchezo wa pili wa wanaume utachezwa saa mbili usiku. Amesema katika mchezo huo Serikali imeweka kiingilio kidogo ili wadau wa soka waweze kuingia na kufurahia miaka 60 ya uhuru wa Tanzania yenye mapinduzi makubwa kwenye sekta mbalimbali. Akifafanua kuhusu kiingili...

DKT.POSSI AFUNGA MASHINDANO YA KITAIFA YA GOFU KWA MTINDO WA KIPEKEE

Image
  Mchezaji chipukizi Isack Daudi kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo akikabidhiwa kombe na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi baada ya kuibuka mshindi wa jumla mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku wa Disemba 5, 2021 akitoa hotuba ya kufunga rasmi mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku wa Disemba 5,2021 akikabidhiwa kanuni za mchezo wa Gofu na Mwenyekiti wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Brigadia Generali Mstaafu, Michael Luwongo baada ya kutangaza nia ya kujifunza mchezo huo. Na. John Mapepele Naibu Katibu Mkuu wa WizarayaUtamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku waDisemba 5, 2021 amefunga rasmi mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kanuni za mchezo huo na Mwenyekiti wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Brigedia Generali Mstaafu, ...

KOMBE LA CANAF 2021 KUBAKI TANZANIA NI LAZIMA , NJOONI TUISHANGILIE TEMBO- BASHUNGWA.

Image
  Na. John Mapepele Waziri mwenye dhamana ya   nchini,  Mhe. Innocent Bashungwa  ametoa wito kwa wadau wa Michezo nchini  kujitokeza kwa wingi leo Disemba 2, 2021 kuishangilia timu ya Tanzania ya soka ya wenye ulemavu (Tembo Warriors) katika  mchezo wake wa nusu fainali na  timu Liberia ili waweze kutwaa kombe la mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa wenye ulemavu CANAF 2021. Mhe. Bashungwa ametoa wito huo leo kufuatia  timu ya Tembo Warriors jana kufuzu mashindano ya dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika Oktoba 2022 nchini Uturuki. "Tunamshukuru Mungu kazi ya kwanza ya kufuzu kwenda  kombe la dunia tumeifikia jana kwa kuwa timu ya kwanza kufuzu, kazi ya leo  tunahakikikisha tunaibamiza  Liberia, ili tufike fainali na kulibakiza kombe nchini ili kuliheshimisha taifa letu nitoe wito  kwa watu wajitokeze kuishangilia kwa wingi na kuipa hamasa timu yetu iendelee kushinda" ameeleza, Mhe. Bashungwa. Aidha, amefafanua kwa...

TANZANIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MCHEZO WA SOKA KWA WENYE ULEMAVU

Image
  .         ******************** Na. John Mapepele Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon mabao 5-0. Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na Kamati Maalum ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri kutokana hamasa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan. Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo tembo ilishinda gol...