Bashungwa Afafanua Mafanikio Ya Sekta Za Utamaduni, Sanaa Na Michezo Kwa Rais Samia
Na. John Mapepele, WSUM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ubunifu wa kuandaa mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo ikiwa ni pamoja na kuandaa Tamasha kubwa la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo linaoanza kesho oktoba 28 hadi 30 mjini Bagamoyo. Rais Samia ameyasema hayo leo Oktoba 27, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam kwenye hafla maalum aliyoiandaa kwa ajili ya kuipongeza Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kutwa Kombe la COSAFA hivi karibuni. “Ili kufanikisha ushindi naomba nitambue TFF, Wizara na Wadau wengine hongereni kwa umoja wenu, najisikia fahari Twiga Stars kushinda ugenini na kuleta kombe nyumbani” amefafanua Mhe. Rais Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu isemayo “Sanaa ni Ajira” lina lengo la kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni wa mtanzan...