Posts

Showing posts from August, 2021

WAZIRI BASHUNGWA AWAPIGANIA WANAMICHEZO KUPATIWA CHANJO DAR

Image
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ,akizngumza na wachezaji wa  timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya  Kidongo chekundu maarufu kama  JK Park jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa aliyevalia jezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) katikati  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mpira wa soka na wachezaji wa timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya  Kidongo chekundu maarufu kama  JK Park jijini Dar es Salaam. ………………………………………………….. Na John Mapepele, WHUSM Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya leo Agosti 28, 2021 imeratibu zoezi la hiari la siku mbili kwa timu za Taifa za michezo na wadau wote wa michezo upatiwa chanjo ya Uviko-19 ji...