Posts

Showing posts from June, 2021

FAINALI ZA KIHISTORIA UMISSETA 2021 ZAUNGURUMA MTWARA

Image
    Mwandishi Maalum, Mtwara Michezo inayoendelea kwenye Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) yanafikia fainali Julai 1, 2021 kwenye viwanja mbalimbali vya mjini Mtwara ambapo mashindano hayo yatafungwa rasmi Julai 2,2021. Kwa mujibu wa Msemaji wa mashindano hayo, John Mapepele fainali ya soka kwa wavulana itakuwa baina ya timu ya Pemba na Mtwara na itachezwa siku ya kufunga mashindano hayo Julai 2, 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu soka utachezwa kesho baina ya timu ya mkoa wa Dodoma na Geita. Amesema mchezo wa Soka kwa upande wa wasichana utakuwa baina ya timu ya mkoa wa Mwanza na Tabora ambao utachezwa mchana Julai 1,2021 ambapo hadi sasa mshindi wa tatu ni mkoa wa Arusha.   Pia fainali ya Mpira wa Pete itakuwa dhidi ya timu ya mkoa wa Mwanza na Songwe Kwa upande wa mpira wa Wavu fainali wasichana itachezwa baina ya mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara wakati wavulana itakuwa kati ya Dar es Salaa...

DKT ABBASI ATAJA WASANII WATAKAOPAMBA UMISSETA

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza kuhusiana na Mashindano ya Umiseta MAUA Sama mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika Mashindano hayo MSANII Chege Chigunda ambaye ni miongoni mwa Wasanii watakaotumbuiza wakati wa Ufunguzi wa MAshindano ya UMISSETA Na John Mapepele, Mtwara Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wakiongozwa na Maua Sama na Chegi wanatarajia kupamba ufunguzi wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yatakayofunguliwa kesho Juni 21, 2021 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (Mb) kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kikamilifu na inaendelea kutoa kipaombele kwenye Sekta ya Sanaa hivyo anawaalika wadau mbalimbali kuja kushuhudia burudani mwanana zinazoendelea kwenye mashindano ha...

WADAU WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA MICHEZO YA OLYMPIC

Image
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo (aliyeshika mfuko) kwenye picha ya pamoja na timu ya riadha na wafanyakazi ya Kampuni ya Ocean Silent Limited baada ya kukabidhiwa  msaada wa vyakula.    Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo akiongea na Vyombo vya Habari akiwataka wadau wa michezo kuendeleza vipaji vya wanamichezo kuanzia kwenye mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Wanariadha wakijipanga kwa ajili ya kushiriki mbio za mita 1500 kwenye mashindano ya UMITASHUMTA yanayoendelea mjini Mtwara yaliyofunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Juni 8, 2021. v    >Serikali yawataka washiriki UMITASHUMTA, UMISSETA Na John Mapepele, Mtwara Mdau wa michezo nchini, Kampuni ya Ocean Silent Ltd, amesema anajitolea vyakula kwa ajili ya kuisaidia timu ya riadha katika kipindi chote kilichobaki wakati timu hiyo inapojiandaa kushiriki mashindano ya Olympic yanayotara...

UMITASHUMTA YATOA SITA KWENDA SLOVENIA MASHINDANO YA DUNIA

Image
  Wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mashindano ya mbio za mita 1500 katika viwanja vya Chuo cha Walimu leo Juni 14, 2021 mjini Mtwara. 1    Mratibu wa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Leonard Thadeo akitoa maelekezo kwa waamuzi na waratibu wa michezo wa mikoa mbalimbali iliyoshiriki mashindano hayo leo Juni 14,2021 mjini Mtwara 1.    Makatibu wakuu wa Wizara (Habari, TAMISEMI, na Elimu) zilizoratibu mashindano ya UMISHUMTA na UMISSETA na Wakurugenzi wakikagua miundombiunu ya mashindano hayo kabla ya kuanza rasmi Juni 7,2021 mjini Mtwara Na John Mapepele, Mtwara Serikali imesema wanafunzi sita watakaofanya vizuri mashindano ya UMITASHUMTA upande wa Riadha yanayoendelea kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu mjini Mtwara watapelekwa katika mashindano ya kimataifa ya Shirikisho la Michezo ya Wanafunzi Duniani (ISSF) yatakayoanza Septemba mwaka huu nchini Slovenia Hayo yasemwa na Mratibu wa UMITASHUMTA na UMISSETA Taifa, Leonard Thadeo wakati akionge...

WASANII WA KIZAZI KIPYA KUPAMBA UMISSETA, UMITASHUMTA

Image
  Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo akifanya  Mahojiano  kwenye kituo cha Redio cha Safari FM mjini Mtwara Na John Mapepele, Mtwara   Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, taarabu na singeli ni miongoni mwa makundi ya wasanii watakaopamba Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) yanayofunguliwa leo Juni 08, 2021 na Waziri Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amebainisha hayo alipofanya mahojiano na Vituo vya Redio mjini Mtwara leo ambapo amewataja wasanii wa kizazi kipya watakaopamba mashindano hayo kuwa ni pamoja na Ibrah kutoka Konde Gang, Beka Flavour, Peter Msechu na Linah Sanga, pia msanii maarufu wa Singeli Dulla Makabila na Mfalme wa taarabu Mzee Yusuf. Amesema mashindano ya mwaka huu yanaanza ...