BODABODA SINGIDA WATOA TAMKO KALI KUELEKEA KUAPISHWA RAIS DKT JOHN MAGUFULI

Mwenyekiti wa madereva na wamiliki wa Bajaji na bodaboda Manispaa ya Singida Ahmed Juma akitoa ufafanuzi wa tamko la kulaani vijana wanaotaka kufanya vurugu Dereva wa Bodaboda Manispaa ya Singida Ramadhani Zuberi akitoka ufafanuzi kwa waandishi ambao hawapo pichani kupinga na kulaani maandamano ya vijana ambao wanataka kutumika kuvuruga amani Sehemu ya madereva wa bodaboda Manispaa ya Singida John Mapepele na Rose Nyangasa, Singida Wamiliki na Madereva wote wa Bajaji Mkoa wa Singida wametoa tamko rasmi la kulaani baadhi ya vijana ambao wameanza kutumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani kuandamana kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, Mwaka huu. Akitoa tamko kwa niaba ya wanachama 2000 wa Mkoa wa Singida kwenye Kituo cha Bajaji Soko Kuu la Mjini Singida, Mwenyekiti wa Madereva na Wamiliki wa Bajaji na Boda boda Manispaa ya Singida, Ahmed Juma amesema umoja wao umepi...