WATUMISHI TUME YA MADINI WATAKIWA KUWA WAADILIFU

Na Greyson Mwase Watumishi wa Tume ya Madini nchini wametakiwa kuwa waadilifu kwenye utendaji wa shughuli zao za kila siku hivyo kuendelea kujenga taswira chanya kwenye Sekta ya Madini. Wito huo umetolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2020 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, *Profesa Shukrani Manya* kwenye ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua shughuli za Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mbeya pamoja na kutatua changamoto mbalimbali. Katika ziara yake Profesa Manya ameambatana na Meneja Utawala na Rasilimaliwatu, Gift Kilimwomeshi na kupokelewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Godson Kamihanda. Akizungumza na watumishi hao, Profesa Manya amesema kuwa, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imejipanga katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye Sekta ya Madini, na kusisitiza kuwa uadilifu kwenye utendaji kazi unahitajika ili kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye Sekta ya Madini. Katika hatua nyingine, Profesa Man...